Paris,Ufaransa.
WACHEZAJI wa Paris St-Germain (Pichani) wakipongezana baada ya usiku huu kuibomoa Monaco mabao 5-0 katika mchezo wa nusu fainali wa kuwania kombe la ligi uliochezwa kwenye dimba la Parc des Princes.
Mabao yaliyoipa ushindi Paris St-Germain katika mchezo huo ambao Monaco walipumzika sehemu kubwa ya kikosi chake cha kwanza yamefungwa na Julian Draxler,Edinson Cavani,Blaise Matuidi,Safwan Mbae aliyejifunga na Marquinhos.
Ushindi huo umeipeleka Paris St-Germain fainali kwa mara ya tatu mfululizo na sasa itacheza na Angers huko Stade de France Mei 27 mwaka huu.
Angers imefuzu fainali kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60 baada ya Jumanne usiku kuifunga Guingamp mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment