Farid Miraji,Dar Es Salaam.
Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji imemfungia mechi mbili beki wa Simba, Abdi Banda kwa kosa la kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Aprili 2, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Hatua hiyo inamaanisha Banda sasa yuko kuendelea kuichezea Simba, kwani tayari amekwishakosa mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC timu yake ikishinda 3-2 na dhidi ya Toto Africans wakioa sare ya 0-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kama pia ilibaini Banda ambaye hakupewa adhabu yoyote na refa kwa sababu hakuona tukio hilo.Sasa Banda amekuwa huru na anaweza kutumika kwa michezo ijayo ya ligi kuu ambayo klabu yake ya Simba SC imebakiza michezo mitatu.
0 comments:
Post a Comment