Leceister,England.
ULE mwanzo mzuri wa safari ya kwanza ya Leicester City kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya hatimaye umefikia mwisho baada ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu England kutupwa nje ya michuano hiyo na kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali uliochezwa huko King Power,jijini Leceister.
Wageni Atletico Madrid ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Saul Niguez kufunga kwa kichwa katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza kabla ya Jamie Vardy kuisawazishia Leicester City katika dakika ya 61 na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Sare hiyo imeifanya Atletico Madrid ifuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 baada ya kushinda mchezo wa awali kwa bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Antoine Griezmann.
0 comments:
Post a Comment