Barcelona, Hispania.
KOCHA wa Osasuna,Petar Vasiljevic amesema kikosi chake kitahitaji msaada wa ziada leo usiku kuweza kumzuia Lionel Messi pale kitakaposhuka dimbani Camp Nou kucheza na Barcelona katika muendelezo wa michezo ya ligi ya La Liga.
Vasiljevic ambaye juzi Jumapili alikuwa sehemu ya mashabiki waliomshuhudia Messi akifunga mabao mawili dhidi ya Real Madrid,Santiago Bernabeu amewataka wachezaji wake kutoonyesha uoga licha ya ukweli kwamba kichapo kutoka kwa Barcelona kitawafungulia rasmi milango ya kushuka daraja.
Tayari nimeshasema kwamba tunahitaji mpango madhubuti kuweza kumzuia Messi leo.Wachezaji wangu wameniambia tunahitaji kubeba pingu pamoja na bastola ili kumzuia Messi.Amesema Vasiljevic.
0 comments:
Post a Comment