728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 14, 2017

    MNAZINGUA:Mashabiki Mbeya City waijia juu timu yao


    Mbeya,Tanzania.

    MASHABIKI wa Mbeya City wameijia juu timu yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuchoshwa na mwenendo mbovu wa timu hiyo kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inayoendelea kutimua vumbi lake.

    Kwa nyakati tofauti Mashabiki hao wamekiri kuvunjika moyo hasa baada ya jana Alhamis timu hiyo Kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na African Lyon hali iliyoifanya timu hiyo kuambulia pointi tatu pekee kwenye michezo yake minne iliyopita.

    Mashabiki hao wametoa sababu mbili ambazo wanadhani ndizo zinazoikwamisha timu hiyo kufanya vizuri kama ilivyokuwa hapo zamani.

    Wamesema kusuasua kwa timu yao kumetokana na kusajili wachezaji wengi ambao siyo wazawa wa mkoa wa Mbeya hali inayowafanya wasiwe na uchungu na timu hiyo zaidi ya kuweka mbele maslahi yao.

    Mashabiki hao wameongeza kuwa zamani Mbeya City ilikuwa ikifanya vizuri kutokana na kusheheni wachezaji wengi wenye asili ya mkoa huo, ambao walikuwa wanacheza kwa mapenzi na uchungu mkubwa.

    Sababu nyingine ambayo Mashabiki hao wameitoa ni kwamba makocha wa timu hiyo Mzambia,Kinnah Phiri na msaidizi wake, Mohammed Kijuso ambaye ni mzawa wamekosa jipya la kuifanyia timu hiyo na wangependa kuona uongozi ukiwatimua kazi mara moja kwani tangu walipopewa mikoba ya kuinoa timu hiyo hakuna mafanikio yoyote yale ya maana ambayo wameiletea timu hiyo maarufu kama Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya. 

    Kwa sasa Mbeya City iko katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu bara ikiwa imejikusanyia pointi 33 baada ya kucheza michezo 28.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MNAZINGUA:Mashabiki Mbeya City waijia juu timu yao Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top