728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 14, 2017

    Lucas Alcaraz kocha mpya Algeria


    Algiers,Algeria.

    ALGERIA imemteua Mhispania, Lucas Alcaraz kuwa kocha mkuu mpya wa timu yake taifa.

    Alcaraz mwenye umri wa miaka 50 amepewa kibaria hicho zikiwa ni siku nne tu zimepita tangu atimiliwe kuifindisha Granada baada ya kuweka makazi ya kudumu mkiani mwa msimamo wa ligi ya La Liga.

    Uteuzi huo Alcaraz umekuja kama mshituko kwa mashabiki wa Algeria kwani awali kulikuwa na taarifa kuwa Mhispania mwingine, Joaquin Caparros ndiye aliyetarajiwa kupewa kibarua hicho kilichokuwa wazi tangu mwezi Januari baada ya Mbelgiji Georges Leekens kubwaga manyanga.

    Leekens alibwaga manyanga baada ya Algeria kung'olewa mapema kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon na Cameroon kuibuka mabingwa baada ya kuifunga Misri kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

    Jukumu kubwa alilopewa Alcaraz ni kuhakikisha Algeria inafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia la mwakani pamoja na ile ya AFCON ya mwaka 2019 itakayofanyika nchini Cameroon.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Lucas Alcaraz kocha mpya Algeria Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top