Sunderland, England.
WABISHI Newcastle United wamerejea ligi kuu England baada ya jana Jumatatu usiku kuwashushia kisago cha mbwa mwizi Preston North End kwa kuwafunga mabao 4-1 huko St James' Park.
Mabao yaliyoirejesha Newcastle United ligi kuu England yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania,Ayoze Perez aliyefunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili.
Mabao mengine yamefungwa na Christian Atsu pamoja na Matt Ritchie aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya nahodha wa Preston North End,Paul Gallagher kushika mpira kwa makusudi ndani ya eneo la boksi.Bao la kufutia machozi la Preston North End limefungwa na Jordan Hugill.
Ushindi huo umeirejesha Newcastle United ligi kuu England zikiwa ni siku 348 zimepita tangu iliposhuka daraja msimu uliopita pamoja na vilabu vya Norwich City pamoja na Aston Villa.
0 comments:
Post a Comment