:Simba Iko juu ya Azam
:Bocco kiboko ya Simba
Kuelekea mechi ya nusu fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho maarufu kama Tff azam sports federation cup (ASFC) utakaochezwa Kesho kwenye uwanja wa taifa rekodi inaibeba Simba ila Bocco ni hatari zaidi kwa Simba.
Timu za Azam na Simba zimefika Hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mechi tatu ikiwa mechi ya kwanza ni ya 32 bora, mechi ya pili ni ya 16 bora na ya tatu ni ule wa robo fainali .
Hii ndio safari ya azam Fc na Simba Kwa kombe la shirikisho maarufu kama ASFC
AZAM FC
Azam Wamecheza mechi zao zote tatu katika Dimba lao Azam Complex (Chamazi) Katika Hatua ya 32 bora walianza na timu ya daraja la pili Cosmopolitan ya Dar na kuifunga Kwa mabao matatu Kwa bila (3-0) magoli ya Azam yakifungwa na John Bocco, Shabani Iddi na Joseph Mahundi, Katika Hatua ya 16 Bora azam Fc walipambana na Mtibwa Sugar ya Morogoro na kuifunga Kwa bao moja kwa bila (1-0) goli la Winga Ramadhan Singano, Katika Hatua ya robo fainali Azam Fc wakapangwa na Ndanda Fc ya Mtwara , Mchezo huo uliofanyika Katika Dimba la Chamazi Azam Fc wakatoa kipigo cha mabao matatu Kwa moja (3-1) mabao ya yakifungwa na Shabaani Iddi mawili (2) na Ramadhan Singano
SIMBA SC
Timu ya Simba SC ilianza safari yao katika raundi ya tano (32-bora) dhidi ya Polisi Dar. Simba walifanikiwa kuifunga Polisi kwa Mabao mawili Kwa bila (2-0) magoli ya Simba yalifungwa na Pastory Athanas na Mohamed Hussein . Baada ya Simba kuitoa Polisi Dar alifanikiwa kuingia raundi ya sita (16 bora) wakapangwa na African Lyon iliyopo ligi kuu Katika mchezo huo Simba walishida Kwa goli moja kwa bila (1-0) goli la Mshambuliaji Laudit Mavugo. Katika raundi ya Saba (robo fainali) Simba wakapangwa kucheza na timu ya ligi daraja la pili mashali wa Arusha Madini Fc katika uwanja wa Sheikh Abeid Arusha. Katika mchezo huo Goli la Laudit Mavugo lilitosha kuipeleka Simba raundi ya nane (nusu fainali) Katika Ushindi wa bao moja kwa bila (1-0)
Wanaongoza Kwa ufungaji Mwaka huu ASFC
-Shabaani Iddi (Azam) -3
-Laudit Mavugo (Simba) -2
-Ramadhan Singano (Azam) -2
Kuelekea mchezo wa Kesho wa Azam na Simba hizi ndio rekodi zao wamekutana Mara 25 Katika mashindano sita tofauti Simba wakishida Mara 11 Huku Azam akishinda Mara 9 na kutoka sare Mara 5 .
Ligi kuu ya Tanzania (VPL)
Azam na Simba wamekutana Mara 18 Simba wameshida mechi 8 azam Mara 5 na wakitoa sare Mara 5
Mapinduzi Cup
Katika kombe hili wamekutana Mara tatu Azam wakishida mechi zote tatu kama ifutavyo
2011 Nusu fainali
Azam 2-0 Simba
2012 Nusu fainali
Azam 2-2 Simba (Penati 5-4)
2017 Fainali
Azam 1-0 Simba
Kombe la kagame
Katika kombe la kagame wamekutana Mara moja mwaka 2012 Kweye robo fainali na Azam kushinda Kwa mabao 3-1
Ngao ya Jamii
-Hapa walikutana Mara moja mwaka 2012 Simba wakishinda Kwa mabao matatu Kwa mbili (3-2)
Kombe la Ujirani Mwema
Mwaka 2012 Simba na Azam walikutana fainali ya kombe la ujirani mwema na Simba kushinda Kwa penati (4-3) baada ya sare ya mabao mawili Kwa mawili (2-2)
Kombe la ABC SUPER 8
Katika kombe hili mwaka 2012 Simba walikutana na Azam kwenye nusu fainali na Simba kushinda Kwa mabao mawili Kwa moja (2-1)
BOCCO KIBOKO YA SIMBA
kama kuna mchezaji wa kuchungwa Katika mchezo wa Kesho ni nahodha wa Azam Fc ikiwa ameifunga simba mabao kumi na tisa (19) hii ni rekodi nzuri
0 comments:
Post a Comment