London,England.
LIGI KUU nchini England inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini humo.
Baadhi ya michezo itakayochezwa leo itashuhudiwa wabishi Tottenham Hotspur wakiwa nyumbani White Hart Lane kuwaalika AFC Bournemouth huku mabingwa wa msimu uliopita Leicester City wakiwa wageni wa Crystal Palace huko Selhurts Park.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumapili kwa michezo mitatu kuchezwa huku mchezo unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi ni ule utakaozikutanisha Manchester United na Chelsea huko Old Trafford jijini Manchester.
Jumatatu ligi hiyo itaendelea kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo Arsenal watakuwa wageni wa Middlesbrough huko Riverside.
Hii ni ratiba kamili
Jumamosi Aprili 15,2017
8:30 Tottenham Hotspur v Bournemouth
11:00 Crystal Palace v Leicester City
11:00 Everton v Burnley
11:00 Stoke City v Hull City
11:00 Sunderland v WestHam United
11:00 Watford v Swansea City
1:30 Southampton v Manchester City
Jumapili Aprili 16,2017
9:30 West Bromwich Albion v Liverpool
12:00 Manchester United v Chelsea
Jumatatu Aprili 17,2017
4:00 Middlesbrough v Arsenal
0 comments:
Post a Comment