London,England
DIEGO Costa ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu baada ya kufikisha nusu karne (mabao 50) ligi kuu nchini England.
Costa,27, amefikisha idadi hiyo ya mabao na kuivuka kwa bao moja zaidi baada ya jana Jumanne usiku kuifungia Chelsea mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Southampton.
Costa amefikisha idadi hiyo ya mabao katika michezo 85 ikiwa ni mapema zaidi ya mshambuliaji wa zamani wa Liverpool,Luis Suarez aliyefikisha idadi hiyo katika michezo 86.
Katika msimu wake wa kwanza Costa aliifungia Chelsea mabao 20.Msimu wa pili mabao 12 huku msimu huu akiwa tayari ameshapachika mabao 19.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji waliofunga mabao 50 mapema zaidi ligi kuu England.
0 comments:
Post a Comment