728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 20, 2017

    Ligi kuu bara kuendelea tena leo


    Shinyanga,Tanzania.

    LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo mmoja wa ligi hiyo kuchezwa. 

    Stand United maarufu kama Chama la Wana watakuwa kwenye dimba lao la nyumbani la CCM Kambarage mkoani Shinyanga kuwaalika Wanakuchele,Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara.

    Timu hizo zinaingia kwenye mchezo wa leo zikiwa zimetofautiana kwa alama mbili pekee.Stand United wako nafasi ya 8 wakiwa na alama 32 huku wapinzani wao Ndanda FC wakiwa katika nafasi ya 13 baada ya kujikusanyia alama 30.Timu zote zimecheza michezo 27.

    Stand United wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar katika mchezo uliopita huku Ndanda FC wao wanaingia CCM Kambarage wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 4-2 na Mwadui FC katika mchezo uliopita huko Mwadui Complex.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi kuu bara kuendelea tena leo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top