728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 25, 2015

    YANGA SC YAJIPANGA KUMNASA KIUNGO MKABAJI WA APR ILI KUJIWEKA SAWA NA MICHUANO YA AFRIKA

    Yanga imesema inapambana kuhakikisha inamsajili kiungo mkabaji wa APR, Yannick Mukunzi ili kujiimarisha katika michua ya kimataifa msimu ujao.

    Mukunzi anayevaa jezi namba sita, anafanya vizuri kwenye kikosi cha cha APR inayomiliki na Jeshi la Rwanda ambapo sasa viongozi wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha inamsajili kiungo huyo.
    Mmoja wa mabosi wa Yanga anayeshughulikia usajili, amesema kuwa, Mukunzi anaweza kusajili ili kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite kutokana na gharama za kuwa naye kuwa kubwa.

    “Tunataka kumsajili Mukunzi atusaidie katikati kwani tumeo kuna tatizo katika kiungo mkabaji na hata Twite anatumik ndivyo sivyo.

    “Hata gharama za kuwa na Twi ni kubwa mno kwani kila mwaka tunapaswa kuilipa FC Lupopo do 10,000 (Sh milioni 20) kama mkataba unavyosema, kwa hiyo k tukifanikiwa kumsajili Mukuzi atachukua nafasi ya Twite ikishindikana basi,” alisema b huyo.

    Hata hivyo awali kumekuwa na taarifa kwamba, Yanga inasaka beki kutoka katika Kombe la Kagame ili aongeze nguvu katik michuano ya kimataifa.

    Ukiacha Cannavaro na Yondani mabeki wengine wa kati wa Yang ni Pato Ngonyani, Rajab Zahir anayetarajiwa kutolewa kwa mko na kiraka Mbuyu Twite.

    Wakati huohuo, straika wa Kpah Sherman anatarajiwa kuondoka kesho Jumapili kwenda Afrika Kusini kufanya vipimo katika Klabu ya Mpumalanga Black Aces ili aweze kujiunga nayo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAJIPANGA KUMNASA KIUNGO MKABAJI WA APR ILI KUJIWEKA SAWA NA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top