728x90 AdSpace

Tuesday, July 28, 2015

CECAFA:GOR MAHIA MKIZINGUA TENA MTATUKOMA!!

Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limeiandika barua ya onyo klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu katika michezo yake miwili ya kwanza.

Katika barua hiyo ya Cecafa kwenda kwa Gor Mahia, imeutaka uongozi huo kuhakikisha kocha wake Frank Nutal na kikosi kizima kinafuata taratibu za mashindano na kanunu zilizopo zinazoongoza michuano hiyo.

Kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo (LOC) iliwasilisha malaliko kwa uongozi wa Cecafa juu ya tabia ya utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na kocha mkuu wa Gor Mahia, na kitendo cha kuvunja kitasa cha mlango ili kuingia uwanjani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: CECAFA:GOR MAHIA MKIZINGUA TENA MTATUKOMA!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown