728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 30, 2015

    HATARI SANA:FLUMINENSE YAMTEMA RONALDINHO KISA ZOMEA ZOMEA YA MASHABIKI

    Fluminense imevunja mkataba na Ronaldinho ikiwa ni miezi miwili tu tangu nyota huyo wa zamani wa dunia ajiunge na klabu hiyo akiwa kama mchezaji huru.

    Fluminense imefikia hatua hiyo baada ya Ronaldinho mwenyewe kutaka mkataba wake uvunjwe baada ya mambo kuonekana kumuendea kombo nyota huyo wa zamani wa vilabu ya PSG,FC Barcelona na AC Milan.

    Taarifa za ndani zinasema Ronaldinho hakuonekana hakufurahishwa na kitendo cha mashabiki wa klabu hiyo kumzomea mara kwa mara baada ya kushindwa kuibeba Fluminense katika michuano mbalimbali.

    Ronaldinho ameichezea Fluminense jumla ya michezo nane huku akishindwa kupika wala kufunga bao lolote miamba hiyo ya Rio di Janeiro aliyoikuta ikiongoza ligi na sasa ikiwa hatarini kushuka daraja baada ya kuporomoka mpaka nafasi ya kumi na mbili.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATARI SANA:FLUMINENSE YAMTEMA RONALDINHO KISA ZOMEA ZOMEA YA MASHABIKI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top