Kinda wa Manchester United Mbrazil Andreas Pereira amemshukuru kiungo wa klabu hiyo Juan Mata kwa kumpa nafasi ya kupiga faulo iliyozaa goli la pili katika mchezo ambao Manchester United iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Ipswich Town katika mchezo wa raundi ya 3 wa Capital One jana usiku.
Baada ya mchezo,Pereira ameiambia MUTV
"Namshukuru sana Juan Mata kwa kunipa nafasi ile na kufanikiwa kufunga goli langu la kwanza.Nilimuomba mpira na akanipa bila wasiwasi kwakuwa ananiamini.Mata anaujua uwezo wangu katika kupiga faulo kwani tumekuwa tukifanya mazoezi pamoja."
Pereira aliongeza "Nimefurahi kufunga usiku wa leo ni ndoto iliyotimia.Naishukuru klabu yangu,kocha wangu na familia yangu."
0 comments:
Post a Comment