Umesikia Bayern Munich imeshinda kwa mabao 5-1 dhidi ya Wolfsburg, lakini haikuwa kazi rahisi.
Huyu jamaa Robert Lewandowski alikuwa benchi, huku ikionekana kama wenyeji Bayern Munich wakizama katika mechi ya Bundesliga baada ya Wolfsburg kupata bao la mapema.
Kocha Pep Guardiola akaona bora kumuingiza mkali huyo wa mabao ambaye ameonyesha kweli anaweza.
Lewandowski alianza kazi ya kupachika bao moja baada ya jingine na ndani ya dakika 9 tu, tayari alikuwa ameishafunga matano na kuiwezesha timu yake kushinda kwa mabao 5-1.
Bao la kwanza alifunga katika dakika ya 51, halafu akaendeleza hivi, la pilidakika ya 52, tena katika dakika ya 55, akaongeza dakika ya 57, kabla ya kupiga la tano katika dakika ya 60.
Huyu mtu ni hatari, unakumbuka katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Borussia Dortmund aliwahi kupiga mabao manne.
Huyu mtu ni hatari, unakumbuka katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Borussia Dortmund aliwahi kupiga mabao manne.
0 comments:
Post a Comment