728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 22, 2015

    FERGUSON:MOYES HAKUWA CHAGUO LANGU LA KWANZA,AELEZA ALIVYOMKOSA MOURINHO


    Meneja wa zamani wa Manchester United Mscotland Sir Alex Ferguson amefichua kuwa Mscotland mwenzie David Moyes hakuwa chaguo lake la kwanza katika kukalia kiti cha kuinoa Manchester United pindi alipokuwa akijiandaa kustaafu mwaka 2013.

    Ferguson ameyasema hayo katika kitabu chake kipya kiitwacho "Leading" na badala yake alitaka Muhispania Pep Gurdiola ndiyo awe mrithi wake namba moja.Ferguson alitaka Gurdiola awe mrithi wake akiamini ndiye mtu sahihi wa kuifanya kazi aliyoianza miaka mingi iliyopita.
    Bayern Munich's coach Pep Guardiola shouts
    Ferguson alionekana kupendelea zaidi kurithiwa na Muhispania huyo baada ya kuambulia vipigo mara mbili toka kwa Gurdiola katika fainali za ligi ya mabingwa Ulaya 2009 na 2011 akiwa na FC Barcelona.
    Amesema "Nilipata nafasi ya kupata chakula cha usiku na Pep Guardiola huko New York mwaka 2012 lakini sikuweza kumwambia pendekezo langu kwani wakati huo suala la kustaafu kwangu lilikuwa bado haliko katika ajenda.Nilichomwambia ni kuwa anipigie simu kabla hajaamua kujiunga na klabu yoyote ile lakini kwa bahati mbaya hakunipigia simu wakati akiamua kujiunga na Bayern Munich kuchukua nafasi ya Jupp Heynckes" 

    Ferguson anaendelea kubainisha jinsi alivyompata Moyes
    David Moyes
    "Niliamua kumopendekeza Moyes baada ya makocha wengine kuonekana kuwa hawawezi kupatikana kwa wakati huo.Jose Mourinho alikuwa tayari ameshafanya mawasiliano ya kurejea Chelsea akitokea Real Madrid na nafasi yake ilipaswa kuzibwa na Carlo Ancelotti,Jurghen Klopp alikuwa na furaha Dortmund wakati Luis Van Gaal alikuwa akiinoa Uholanzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FERGUSON:MOYES HAKUWA CHAGUO LANGU LA KWANZA,AELEZA ALIVYOMKOSA MOURINHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top