Liverpool huenda ikaingia dimbani siku ya jumamosi kuivaa Aston Villa bila ya mshambuliaji wake mahiri Christian Benteke anayesumbuliwa na maumivu ya misuli.
Benteke,24 aliyejiunga na Liverpool akitokea Aston Villa alitolewa uwanjani katika mchezo wa jumapili baada ya kugongwa na mchezaji mmoja wa Norwich City katika mchezo ulioisha kwa sare ya goli 1-1.
Kwa mujibu wa Liverpool Echo,Benteke ana asilimia kubwa za kuukosa mchezo dhidi ya klabu yake ya zamani ya Aston Villa aliyofanikiwa kuifungia magoli 49 katika michezo 100 tangu alipojiunga nayo 2012 akitokea Genk ya Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment