728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 22, 2015

    CHUNGA SANA:NEYMAR AMCHONGEA COUTINHO BARCELONA KIAINA


    Barcelona,Hispania.

    Neymar ametoa kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni kuiambia FC Barcelona ianze kumtupia jicho la kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho.

    Neymar ambaye anafahamika kwa kuwa na urafiki wa karibu sana na Coutinho na wanacheza pamoja katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil anaamini kuwa Coutinho ana kila kitu kinachotakiwa na FC Barcelona.

    Neymar amesema "Nadhani kuna wachezaji wengi wenye ubora mzuri wa kuweza kuichezea FC Barcelona.Mmoja wao ni [Philippe] Coutinho..Ni mchezaji mzuri na aina ya soka lake linaendana sawia na FC Barcelona".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHUNGA SANA:NEYMAR AMCHONGEA COUTINHO BARCELONA KIAINA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top