London,England.
Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuwa imemfanyia majaribio kipa wa zamani wa AC Milan Marco Amelia kabla ya kumsajili hivi karibuni kuziba nafasi ya kipa majeruhi Thibaut Courtois.
Chelsea imemgeukia kipa huyo mwenye miaka 33 baada ya kubaki na makipa wawili tu kikosini ambao ni Asmir Begovic na Jamal Blackman kufuatia kipa wake namba moja Thibaut Courtois kupata jeraha la goti litakalomuweka nje ya dimba mpaka mwezi disemba.
Ikiwa Amelia atafuzu majaribio hayo atajiunga na Chelsea kwa mkataba mfupi akiwa kama mchezaji huru baada ya kutoswa na AC Milan misimu miwili iliyopita kisha akatua klabu ya Seria B ya Rocca Priora ambayo nayo ilimtema msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment