Oussama Tannane.
Eindhoven, Uholanzi.
Wakati bado dunia haijasahau tukio la wiki hii mlinzi wa PSV Eindhoven ya Uholanzi Mmexico Hector Moreno ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mahiri katika kucheza rafu za hatari mara baada ya jana jumamosi kumuumiza vibaya winga wa Heracles Almelo, Oussama Tannane.
Moreno ambaye siku ya jumanne ya wiki hii alimchezea rafu mbaya na kumvunja mguu mara mbili mlinzi wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw,jana jumamosi katika mchezo wa ligi ya Eredivisie alimchezea rafu nyingine mbaya safari hii ikiwa kwa winga Tannane,21 na kusababisha nyota huyo Muholanzi kutolewa nnje ya uwanja akiwa kwenye machera hajitambui.
Moreno alikuwa akijaribu kuumiliki mpira ulionekana kumzidi ujanja ndipo Tannane alipoupitia kitendo kilichofanya mlinzi huyo wa kimataifa wa Mexico kufanya madhambi hayo.
0 comments:
Post a Comment