Kocha Jose Mourinho amethibitisha kuwa Chelsea itavaana na Arsenal jumapili hii bila ya nyota wake wawili muhimu baada ya kukumbwa na majeruhi.
Nyota hao ni Pedro Rodriguez na Willian.Pedro aliumia katika mchezo dhidi ya Everton ulioisha kwa Chelsea kufunga 3-1 huku Willian yeye akipata majeraha ya misuli katika mchezo wa jana usiku wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Macabi Tel Aviv.
Akifanya mahojiano baada ya mchezo dhidi ya Macabi Mourinho amesema Willian hatakuwepo katika mchezo huo wa ligi kuu huku Pedro akiwa na asilimia ndogo sana za kucheza mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment