Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake wa ulinzi Mfaransa Francis Coquelin kupata jeraha la goti siku ya jumamosi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea katika dimba la Stamford Bligde.
Coquelin alipata jeraha hilo katikati ya kipindi cha kwanza baada ya kushuka vibaya akitoka kucheza mpira wa kichwa hali iliyopelekea apatiwe matibabu ya haraka kutoka kwa madaktari wa Arsenal lakini muda ulivyozidi kwenda ndivyo goti lilivyozidi kumsumbua na kumfanya kocha Arsene Wenger kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Calum Chambers.
Kufuatia jeraha hilo Coquelin hatacheza mchezo wa kombe la ligi siku ya jumatano dhidi ya Tottenham huko Whitehate Lane na pengine michezo zaidi kwani taarifa zaidi zitatoka baadae.
0 comments:
Post a Comment