September 27 katika mechi kati ya Azam FC dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa
katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi,
nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso alimfanyia kitendo
cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco, licha ya kuwa
muamuzi hakuona ila kupitia picha za mnato na kanda za video tukio hilo
lilinaswa na kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi amethibitisha
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mchezaji aliyefanya kitendo hicho, Malinzi
amethibitisha hilo kupitia account yake rasmi ya twitter. Lakini hii
sio mara ya kwanza kwa beki na nahodha wa Mbeya
City Juma Nyoso kufanya
kitendo hicho, alishawahi kumfanyia Elias Maguli na kupewa adhabu ya kufungiwa mechi nane
mwanzo mwa mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment