Mino Raiola ambaye ni wakala wa kiungo wa Juventus Paul Pogba ameibuka na kumpinga kocha wa zamani wa Manchester United Alex Ferguson aliyedai kuwa hampendi Raiola kwakuwa alishawishi Pogba kuondoka Manchester United mwaka 2012.
Raiola amejibu mapigo hayo baada ya Ferguson kuandika katika kitabu chake kiitwacho Leading kuwa kuna mawakala wawili anaowachukia huku mmoja wao akiwa ni Mino Raiola.Raiola alimshawishi pogba agomee mkataba mpya wa kubaki Manchester United na badala yake aende zake Juventus.Raiola pate pesa za bure kwani Pogba alikuwa amemaliza mkataba wake.
Raiola amesema "Feguson hajui anachokiongea.Maneno hayo hayaiathiri kazi yangu katika njia hasi bali ni kama uthibitisho kuwa naijua kazi yangu vizuri.Leo Pogba ana thamani inayokaribia paundi milioni 100.
"Nilifanya kile nilichoona kuwa ni chenye faida kwa mchezaji wangu,ningetaka faida yangu mwenyewe basi ningeacha Pogba abaki Manchester United.Nilichokifanya ni kuweka maslahi ya Pogba mbele tukafikia maamuzi na kukahamia Turin.Labda Ferguson anawapenda watu wanaomtii.Kutoka katika nukuu yake,nadhani Ferguson bado hafahamu kuwa Pogba ni nani.
"Ferguson alikuwa ni kocha mzuri lakini pia makocha wazuri nao kuna wakati wanakosea mambo"
0 comments:
Post a Comment