Mlinda mlango wa Arsenal aliyeko kwa mkopo katika klabu ya AS Roma Wojciech Szczesny anatarajiwa kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha wiki sita baada ya kuteguka kidole cha mkono wake wa kushoto.
Szczesny,25 aliteguka kidole hicho baada ya kugongana na mshambuliaji wa FC Barcelona Luis Suarez wakati wakigombea mpira katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa Ulaya juzi katika dimba la Stadio Olympico ambapo matokeo yalikuwa sare ya goli 1-1.
0 comments:
Post a Comment