STRAIKA wa Simba anayecheza kwa mkopo katika Klabu ya KCB ya nchini Kenya, Paul Kiongera, amepata kura nyingi za mashabiki kama mchezaji bora wa mwezi Agosti.
Kiongera licha ya kutolewa kwa mkopo na Simba kwa madai ya kuwa majeruhi ni mmoja wa washambuliaji wanaotisha katika Ligi ya Kenya kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao.
Mshambuliaji huyo aliwapiku wenzake wa timu nyingine ambapo yeye alipata asilimia 60.21, akifuatiwa na George Mandela wa Muhoroni Youth aliyepata asilimia 21.21, huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Lwamba Bebeto aliyepata asilimia 9.89.
Akizungumzia furaha yake hiyo, Kiongera alisema tuzo hiyo ya uchezaji bora wa mwezi Agosti ina maana kubwa kwake na timu yake kwa ujumla.
“Tuzo hii ina maana kubwa kwangu na kwa timu yangu kwa ujumla.Inamaanisha kwamba mashabiki wanaukubali uwezo wangu na sasa natakiwa kujituma zaidi.
“Hii pia inamaanisha kuwa timu yangu inayo wachezaji wazuri kwani tuzo hii sijaichukua kama binafsi yangu, ni timu nzima kwa ujumla,” alisema.(CHANZO:BINGWA)

0 comments:
Post a Comment