728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, September 26, 2015

    TWITE: JAMANI KILA SIKU TUNAFUNGWA SISI TU, NIMECHOKA AISEEE

    Beki kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite amesema amechoshwa kufungwa na Simba kila mara, hivyo leo vyovyote itakavyokuwa ni lazim timu yake ishinde.

    Simba na Yanga zinacheza mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa huku Wanajangwani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa mwisho katika ligi zilipokutana Machi mwaka huu.

    Twite amesema yeye pamoja na wenzake wamechoshwa na vipigo kutoka Simba na sasa wameamua kuwageuzia kibao.

    Mara ya mwisho kwa Yanga kuifunga Simba ilikuwa Mei 18, 2013 ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Ta chini ya Kocha Ernie Brandts r wa Uholanzi.

    “Msimu huu lazima tuifunge Simba iwe isiwe kwani tumechoka na uteja, hivyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda, naamini kambi yetu ya Pemba itatusaidi.

    “Kikosi chetu kizuri na tunahitaji kushinda mechi zetu zote zilizo mbele ili kuweza kutetea ubingwa wetu,” alisema Twite anayemudu kucheza kiungo pia beki wa kulia hata katikati



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TWITE: JAMANI KILA SIKU TUNAFUNGWA SISI TU, NIMECHOKA AISEEE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top