728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 28, 2015

    KISA KICHAPO CHA JUZI,SIMBA YAMSHTAKI NKONGO TFF


    UONGOZI wa klabu ya Simba jana umeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)kumlalamikia mwamuzi wa mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Yanga, Israel Nkongo, uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

    Katika barua yao ambayo pia imepelekwa kwenye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Simba imemlalamikia mwamuzi huyo kuwa hakuwa sawa katika maamuzi yake na hivyo kuwatoa wachezaji wao mchezoni hali iliyosababisha kuambulia kichapo.

    Katika taarifa yake jana jijini Dar es Salaam, ofisa habari wa klabu hiyo yenye makao makuu yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo, Haji Manara, alisema wao wanakubali matokeo hayo ya dakika 90 za mchezo na kuwapongeza watani wao wa jadi kwa ushindi huo walioupata.

    Alisema pia wanamshukuru Mungu kwa kuweza kumaliza mchezo huo salama kwa kuwa mashabiki wao walionyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi huyo kuharibu mchezo kwa makusudi.

    (BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KISA KICHAPO CHA JUZI,SIMBA YAMSHTAKI NKONGO TFF Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top