Barcelona imepata pigo baada ya nyota na nahodha wake Lionel Messi kupata jeraha la goti katika mguu wake wa kushoto jana jumamosi katika mchezo wa La Liga dhidi ya wageni Las Palmas katika dimba la Camp Nou.Barcelona ilishinda 2-1.
Messi alipata jeraha hilo dakika ya 3 tu ya mchezo baada ya kugongana na mlinzi wa Las Palmas,Pedro Bigas na kulazimika kupelekwa hospitali ya jirani kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Taarifa rasmi kutoka hospitali na kuthibitishwa na klabu ya Barcelona zinasema Messi atakuwa nje kwa kipindi cha wiki 7/8 na hivyo kukosa michezo kadhaa ukiwemo mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayer Leverkusen wiki ijayo,mchezo wa El Classico dhidi ya Real Madrid Novemba 21na michezo miwili ya kufuzu kombe la dunia ambapo Argentina itavaana na Ecuador Octoba 8 na Paraguay Octoba 13.
0 comments:
Post a Comment