Magoli mawili ya mwishoni mwa kipindi cha pili yaliyofungwa na viungo Ramires na Willian yameipatia Chelsea sare ya bao 2-2 dhidi ya Newcastle United katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la St.James Park.
Chelsea ambayo ilionekana kama inaelekea kupoteza mchezo huo ilizinduka baada ya Ramirez aliyetoka benchi kufunga kwa shuti kali akitumia vyema pasi ya Eden Hazard kabla ya Wilian kufunga dakika ya 86 na kuzima magoli ya mapema ya Ayoze Perez na Georginio Wijnaldum.
0 comments:
Post a Comment