Kiungo mshambuliaji wa Royal Eagles, Uhuru Selemani Mwambungu amefunga bao lake la pili akiwa na kikosi chake hicho.
Uhuru amefunga bao lake la pili wakati Royal Eagles ikitwanga Santos bao 4-0.
Hiyo ni mechi ya pili ya Uhuru, mechi yake ya kwanza dhidi ya Amazulu kwa mabao 2-1 yeye akifunga la ushindi.
“Ilikuwa mechi mgumu sana, lakini namshukuru Mungu nimecheza na kufunga,” alisema.(Saleh Ally Blog)
0 comments:
Post a Comment