Iran
Hali ya mambo nchini Iran bado ni tete kwa watu wenye jinsia ya kike.Mbali ya wanawake nchini Iran kuzuiliwa kufanya mambo mengi binafsi lakini hata katika yale yenye maslahi kwa taifa bado wameendelea kuzuiliwa kuyafanya.
Taarifa zilizoifikia Soka Extra kutoka Iran zinasema kuwa nahodha wa timu ya taifa hilo ya wanawake Ardalan hatakwenda na timu hiyo katika michuano ya soka itakayofanyika huko Malysia baada ya mumewe kukataa kusaini nyaraka zitakazo msaidia aweze kupata hati mpya ya kusafiria (passport) kwani iliyopo imekwisha muda wake.
Ardalan,30 maarufu kwa jina la Lady Goal amesema mume wake ambaye ni mwandishi wa habari bwana Mehdi Toutounchi amekataa kusaini nyaraka hizo hivyo hatoweza kusafiri na timu kuelekea Malysia katika michuano ya Asian Football Federation Women's Futsal Championship
"Mume wangu amekataa kusaini nyaraka hizo hivyo siwezi kusafiri.Nadhani serikali ingekuja na suluhisho na kutoa nafasi kwa wanawake kujitetea katika masuala kama haya.Kama mwanamke wa Kiislam nilitaka kuipeperusha vyema bendera ya taifa langu badala ya kusafiri tu kwa starehe na mambo mengine."
Serikali nchini Iran imewapa nguvu wanaume dhidi ya wanawake kwani ili mwanamke aweze kusafiri ni lazima mume akubali.
0 comments:
Post a Comment