London,England.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameachana na mke wake Annie baada ya miaka mitano ya ndoa.
Wawili hao wameachana baada ya uvumi wa miezi kadhaa kuwa uhusiano wao uko hobelahobela huku sababu kubwa ikiwa na kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba kuliko sababishwa na Wenger kuwa bize sana na kazi ya ukocha.
Wenger na Annie, 59, walifunga ndoa mwaka 2010 baada ya kuwa wachumba kwa kipindi kirefu.Mpaka wanaachana tayari wamefanikiwa kuwa na binti mmoja aitwaye Leah,18.Taarifa zaidi zinadai wawili hawajawahi kupiga picha ya pamoja tangu mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment