Unaukumbuka ule moto wa Harry Kane msimu uliopita?Unayakumbuka yale magoli 20 aliyoyafunga katika ligi kuu msimu uliopita?Kwa taarifa yako mpaka sasa Kane hajaifungia Spurs bao lolote lile katika michezo minane mfululizo.
Unajua mashabiki wanasema nini kuhusu hilo?Wanasema tatizo ni jezi namba 10 anayoivaa sasa.Msimu uliopita wakati Kane,22 akifunga mabao jinsi alivyojisikia mgongoni alikuwa akivaa jezi namba 18, sasa tangu ameiacha na kuvaa jezi namba 10 mambo yameanza kumuendea kombo kama yalivyokuwa yakimuendea mtangulizi wake Emmanuel Adebayor ambaye ametupiwa virago vyake hivi karibuni na klabu hiyo ya London.
Je,Kane anasemaje kuhusu jezi namba 10?Kane anasema aliamua kuchukua namba 10 ili aweze kuwa ligendi wa klabu hiyo ya White Hart Lane.
Amesema "Ni namba yenye heshima kubwa sana Spurs.Ukitazama watu alioivaa [ Sheringham, Keane, Hoddle, Ferdinand, Greaves] utajua namaanisha nini"
"Wakati nakua Keane na Sheringham walikuwa mastaa wangu na walikuwa wakivaa namba 10.Hivyo ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu kuivaa namba hii.Namba 18 ilikuwa nzuri, Defoe alinipa lakini nilipogundua namba 10 haina mtu nikaitaka.Naipenda klabu hii na kuvaa jezi namba 10 kwa ni jambo kubwa sana.Nisingeweza kukataa"
0 comments:
Post a Comment