728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 29, 2015

    KUMEKUCHA:NYOTA WATATU YANGA HAOOOO ULAYA


    KLABU ya Yanga imepokea ofa ya kuuza wachezaji wake watatu kutoka katika nchi za Bara la Asia na Ulaya baada ya klabu kadhaa za nchi hizo kuvutiwa na viwango vya uchezaji wao.

    Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, alisema wiki iliyopita kuwa tayari ofa hizo zimewafikia mezani ambapo ofa hiyo inawahusu nyota wao wawili wa kigeni na mmoja akiwa mzawa, lakini akisita kuwataja majina kwa madai ni mapema kufanya hivyo.

    “Tumepokea ofa nono sana ambayo kama tutakubali kuwauza wachezaji hawa watatu, tutakuwa mbali zaidi kiuwezo wa fedha,” alisema Tiboroha.

    Alisema dili hilo Dola za Marekani 900,000 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 1.8.
    Alisema wakifanikiwa kuwauza wachezaji hao, klabu yao itakuwa imejikomboa kiuchumi kwa kiasi kikubwa kutokana na kuingiza fedha hizo ambazo zitatumika kwa ajili ya kukijenga zaidi kikosi chao kuanzia ndani hadi nje ya uwanja.


    Alisisitiza moja ya malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi kimataifa na nyumbani, hivyo wameweka mpango mkakati wa kudumu kuhakikisha Kocha Mkuu wao, Hans van der Pluijm katika programu zake za ufundishaji anazingatia mambo hayo mawili.


    “Tumepania vilivyo kuweka historia, tumemwambia Hans na benchi lake la ufundi kuanza mapema maandalizi ya michuano ya kimataifa,” alisema Tiboroha.

    (Gazeti la Bingwa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUMEKUCHA:NYOTA WATATU YANGA HAOOOO ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top