REKODI aliyoweka mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi anayekipiga Azam FC, Didier Kavumbagu ya kufunga bao zaidi ya moja katika mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara imeshindwa kuvunjwa.
Kavumbagu aliweka rekodi ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-1 msimu uliopita Azam walipowagaragaza Polisi Morogoro ambapo msimu huu hakuna mchezaji aliyeweza kufanya hivyo.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Mrundi huyo alifanikiwa kufunga mabao hayo dakika za 15 na 90, huku lile la tatu likifungwa na Aggrey Morris dakika ya 23.
Kwenye ligi ya msimu huu iliyoanza wikiendi iliyopita, jumla ya mabao 12 yamefungwa huku wachezaji hao wakishindwa kufunga zaidi ya bao moja na kumuacha Kavumbagu kuendelea kuringia rekodi yake.
Tatizo kubwa ambalo linaonekana msimu huu ni baadhi ya washambuliaji kukosa mabao ya wazi na hii ni kutokana na papara hasa wanapolikaribia eneo la hatari la wapinzani wao.
(Kwa habari kamili usikose kujipatia nakala yako ya Gazeti la DIMBA Leo.)
0 comments:
Post a Comment