728x90 AdSpace

Sunday, September 27, 2015

MASIKINI JUVENTUS YAENDELEA KUWA KIBONDE ITALIA,YAGONGWA NA NAPOLI,IMEVUNA POINTI TANO TU KATIKA MECHI SITA

Napoli,Italia.

Juventus imeendelea kuwanyong'onyesha mashabiki wake baada ya usiku wa kuamkia leo kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Napoli katika muendelezo wa michezo ya Seria A.

Juventus iliyokuwa mgeni Katika dimba la Estadio San Paolo ilionyesha mapema kuushindwa muziki wa Napoli baada ya kuwa nyuma kwa magoli mawili ya Lorenzo Insigne na Gonzalo Higuain kabla ya kujipatia goli la kujifutia machozi kupitia kwa kiungo Mario Lemina.

Kufuatia kichapo hicho Juventus huenda ikajikuta katika inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Seria A ikiwa vinara Inter Milan wataifunga Fiorentina leo jumapili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MASIKINI JUVENTUS YAENDELEA KUWA KIBONDE ITALIA,YAGONGWA NA NAPOLI,IMEVUNA POINTI TANO TU KATIKA MECHI SITA Rating: 5 Reviewed By: Unknown