728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 21, 2015

    LA LIGA:BARCELONA MWENDO MDUNDO YAIFUMUA LEVANTE 4-1,MESSI AENDELEA KUTUPIA,PENATI BADO ZAMTESA

    Barcelona,Hispania.

    Magoli mawili ya Lionel Messi na mengine ya Marc Batra na Neymar Jr yameipa FC Barcelona ushindi wa nne mfululizo wa ligi ya La Liga baada ya kuifunga Levante kwa jumla ya magoli 4-1 katika mchezo safi uliopigwa jumapili katika dimba la Camp Nou,Barcelona.

    Messi ambaye alicheza nafasi ya kiungo akiziba nafasi ya Andres Iniesta ambaye ni majeruhi alifunga magoli hayo dakika za 61 (penati) na 90 huku akikosa mkwaju wa penati dakika ya 75 na kupika goli la Batra la dakika ya 50 huku Neymar akifunga goli dakika ya 56 kabla ya Levante kupata goli la kufutia machozi dakika ya 63 kupitia kwa Victor Casadesus.

    Kufuatia ushindi huo FC Barcrelona inaendelea kukaa kileleni mwa ligi ya La Liga ikiwa na pointi 12 ikiicha Real Madrid katika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LA LIGA:BARCELONA MWENDO MDUNDO YAIFUMUA LEVANTE 4-1,MESSI AENDELEA KUTUPIA,PENATI BADO ZAMTESA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top