Magoli mawili ya Bakri Babeker na Francis Coffie yameiwezesha El Merreikh Kuibuka na ushindi wa magoli 2-1dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika uliopigwa jana jumamosi huko Sudan.
El Merreikh ilijipatia magoli hayo dakika za 44 na 80 huku lile la kufutia machozi la TP Mazembe likifungwa na Mtanzania Thomas Ulimwengu dakika ya 77 aliyekuwa ameingia akitokea benchi.
Mchezo wa pili wa nusu fainali ya ligi hiyo kubwa Afrika utachezwa wiki ijayo huko Congo na mshindi atatinga katika fainali.
0 comments:
Post a Comment