Amefunguka.Mshambuliaji raia wa Argentina anayekipiga katika klabu ya FC Napoli ya Italia Gonzalo Higuain ameanzisha vita vya maneno na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo baada ya kudai kuwa nyota huyo siyo lolote siyo chochote kwa Lionel Messi zaidi amejawa na ubinafsina ujivuni tu.
Higuain ambaye aliwahi kuchezea pamoja na Ronaldo katika klabu ya Real Madrid kabla ya kutimka mwaka 2013 asema kucheza pamoja na Ronaldo siyo kitu kama kucheza na Lionel Messi.
Akinukuliwa na gazeti la michezo la Hispania liitwalo Sport ,Higuain amesema: "Ronaldo ni mjivuni sana.Usipomwambia yeye ni bora,hawi rafiki yako.Anaamini yeye ni bora lakini ukweli ni kwamba anabebwa tu.
"Nimecheza na kukaa na Messi katika vyumba vya kubadilishia nguo yuko tofauti sana na Cristiano.Messi siyo mjivuni kabisa"
0 comments:
Post a Comment