MSHAURI wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Abdallah Kibaden, ameipa nafasi kubwa klabu ya Yanga kushinda pambano la watani wa Jadi Simba na Yanga litakalopigwa uwanja wa taifa Jumapili.
Kibadeni aliyewahi kuichezea Simba na baadaye kuifundisha ameiambia Goal, kikosi cha kocha Dylan Kerr, kina mapungufu mengi ukilinganisha na kile cha wapinzani wao Yanga ambao wameonekana kucheza kitimu na kuelewana zaidi.
“Najua utakuwa mchezo mgumu lakini Yanga nawapa nafasi kubwa ya kufanya vizuri endapo watacheza kwenye kiwango chao walichokionyesha kwenye mechi tatu zilizopita, Simba pamoja na kupata ushindi lakini timu bado inamapungufu kinacho wasaidia ni uwezo wa mchezaji mmoja mmoja,”amesema Kibadeni
Kibadeni ambaye ndiyo mchezaji wa kwanza kupiga hat- trick , kwenye pambano la watani wa jadi la mwaka 1977, amesema ameipa nafasi Yanga kwasababu hata ukiangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa timu zote mbili Yanga inawachezaji wengi wenye vipaji na wenye uwezo wa kumiliki mpira tofauti na Simba.
“Zimeanza vizuri lakini nimchezo mgumu na timu ambayo itafanya makosa mengi kwenye mchezo huo ndiyo itakayopoteza mchezo ingawa Yanga bado wanayo nafasi ya kushinda.
Timu hizo zinakutana Jumamosi kwenye uwanja wa taifa Yanga ikiwa inaongoza kwenye msimamo ikiwa na pointi 9 sawa na Simba lakini yenyewe ikiwa na idadi ndogo ya mabao ya kufunga.
0 comments:
Post a Comment