London,England.
Kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki,Arsenal imeripotiwa kupata ahueni baada ya kiungo wake wa ulinzi Francis Coquelin kupona jeraha la goti alilolipata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea wiki mbili zilizopita.
Coquelin amerejea leo asubuhi katika mazoezi ya pamoja na kikosi cha Arsenal katika maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa kesho jumanne wa ligi ya mabingwa dhidi ya Olympiacos utakaopigwa katika dimba la Emirates.Wakati huohuo Arsenal itamkosa katika mchezo huo kiungo wake Mathieu Flamini ambaye alipata jeraha la misuli katika mchezo wa jumamosi wa ligi kuu ambapo Arsenal iliibamiza Leceister City kwa magoli 5-2.

0 comments:
Post a Comment