Sasa ni rasmi kuwa mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili kufuatia jeraha la misuli alilolipata wikiendi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Norwich City na hivyo kukosa mechi tatu muhimu.
Kwa kuanzia Benteke, 24,ataukosa mchezo wa ligi kuu wa jumamosi hii dhidi ya klabu yake ya zamani ya Aston Villa,kisha mchezo wa Octoba 1 wa Europa ligi dhidi ya FC Sion ya Uswisi na mchezo dhidi ya Everton siku tatu baadae.
Kuumia kwa Benteke ni pigo kubwa kwa kocha Brendan Rodgers anayepigana ili kuokoa kibarua chake kutokana na mwenendo mbovu wa klabu kwani tayari ameshampoteza nahodha wake Jordan Henderson ambaye atakuwa nje kwa kipindi cha wiki nane kufuatia kufanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika mfupa katika mguu wake wa kulia.
0 comments:
Post a Comment