London,England.
Chelsea imerejea tena kwenye zama za ushindi baada ya mchana wa leo kuifunga Arsenal goli 2-0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Stamford Blidge.
Chelsea ilijipatia goli la kwanza dakika ya 52 kupitia kwa mlinzi wake Kurt Zouma aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Cesc Fabregas akiwa nje kidogo ya eneo la hatari la Arsenal huku goli la pili likifungwa na Eden Hazard dakika ya 90' na kuipa Chelsea ushindi wa kwanza katika mwezi wa Septemba.
Kadi nyekundu
Arsenal ililazimika kucheza pungufu kwa muda mwingi wa mchezo baada ya nyota wake Gabriel Paulista na Santi Cazorla kulimwa kadi nyekundu baada ya kuwachezea faulo Diego Costa na Cesc Fabregas
0 comments:
Post a Comment