Udinese,Italia.
Antonio Di Natale ameufungua moyo wake na kusema kuwa Alexis Sanchez wa Arsenal ni zaidi ya Neymar Jr wa FC Barcelona.
Di Natale ambaye aliwahi kucheza na Sanchez katika klabu ya Udinese amesema "Neymar na Sanchez wote ni wachezaji wazuri sana.Linapokuja suala la kusema yupi ni bora zaidi ya mwingine hapo ndipo ugumu unapokuja.Kama ningekuwa ni kocha basi ningependa kuwa nao katika kikosi changu lakini nikiambiwa nichague mmoja basi kura yangu itaenda kwa Alexis Sanchez kwani ni mchezaji mkakamavu zaidi kuliko Neymar"
"Alexis ni mchezaji mzuri sana,nimecheza nae Udinese.Nimepata bahati ya kucheza na mabingwa wengi lakini Alexis ni bora zaidi na amethibitisha hilo kwa kufanya vizuri katika vilabu vya Arsenal na Barcelona"
Ni rahisi sana kuonyesha ubora wako katika vilabu vidogo na vya kawaida ambavyo havina presha wala haviko katika ligi kubwa lakini kuonyesha uwezo binafsi katika vilabu vikubwa ni ngumu sana kwani wachezaji wachache tu ndiyo wanaoweza kufanya hivyo"
0 comments:
Post a Comment