London,England.
WAMEFULIA!!Hii ndiyo kauli rahisi unayoweza kuitumia kuielezea klabu ya Manchester City kwasasa baada ya leo mchana kukubali kichapo cha bao 4-1 toka kwa Tottenham Hotspurs katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la White Hart Lane.
Manchester City ilionekana kama ingeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kupata bao mapema kabisa dakika ya 15 kupitia kwa Kevin De Bruyne.
Baada ya kuingia kwa bao hilo Tottenham iliamka na kuanza kulisakama lango la Manchester City kama nyuki na kufanikiwa kupata mabao kupitia kwa Eric Dyer,Harry Kane,Erick Lamela na Toby Alderweireld.
0 comments:
Post a Comment