728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 29, 2015

    MAKALA:NYOSSO ANAHITAJI MSAADA,HUKUMU SIYO SULUHU YA TABIA CHAFU


    Paul Manjale

    Inaitia moyo kuona wadau mbalimbali wa soka nchini wakiungana na kulaani vikali vitendo vya kidhalilishaji anavyoendelea kuvifanya mlinzi wa Mbeya City Juma Nyosso kwa wachezaji wenzie wa ligi kuu Tanzania bara.

    Nyosso ambaye januari mwaka huu alifungiwa michezo minane ya ligi kuu baada ya kuingiza vidole vyake katikati ya makalio ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC Elias Maguli amerudia tena tukio hilo juzi jumapili kwa mshambuliaji wa Azam FC John Bocco katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Chamazi Complex.

    Baada ya tukio hilo ambalo halikuonwa na mwamuzi wa mchezo ule wadau wengi wameonyesha hasira zao juu ya Nyosso na kutaka nyota huyo apewe adhabu kali itakayokuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hizo.

    Binafsi siungani moja kwa moja na wadau wote wanaotaka nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Ashanti na Simba afungiwe kucheza soka na badala yake apatiwe wataalamu wa masuala ya akili (Wanasaikolojia) ili wamsaidie kuondokana na tabia hiyo mbaya.

    Jambo la kujiuliza hapa ni Je, adhabu inasaidia?Kama ndiyo sasa mbona karudia tena?Bila shaka adhabu siyo suluhu ya kubadili tabia ya mtu.Hata kama Nyosso atafungiwa michezo mia moja bila ya kutopatiwa msaada kupitia wanasaikolojia itakuwa ni kazi bure tu adhabu itaisha atarudia tena yale yale.

    Kwa kuhitimisha naomba kuvikumbusha vilabu kuajiri wanasaikolojia ili kuondokana na kadhia kama hii kwani tukio la Nyosso halimchafui na kumuumiza yeye peke yake bali pia linaichafua na kuiumiza Mbeya City na soka letu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAKALA:NYOSSO ANAHITAJI MSAADA,HUKUMU SIYO SULUHU YA TABIA CHAFU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top