Manchester,England.
Alex Ferguson ameendelea kufunguka yaliyomo katika moyo wake kupitia katika kitabu chake kiitwacho Leading baada ya kukiri kushindwa kuwasajili nyota kadhaa mahiri duniani wakiwemo mlinda mlango Peter Cech,Ronaldo de Lima,Didier Drogba na wengineo wengi.
PETER CECH
"Nilienda kumtazama Cech mwaka 2003 akiwa Rennes ya Ufaransa nikashindwa kumsajili kwasababu nilimuona bado ni mchanga sana kuweza kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya England.
DIDIER DROGBA
"Tulikwenda kumtazama Marseille lakini klabu yake ikataka £25m ili imuachie.Wakati tunashauriana tuijue nini cha kufanya Chelsea waliingia na kumwaga pesa na hatimaye
wakamchukua"
"Tulikwenda Brazil kumsajili Ronaldo de Lima mwaka 1994 wakati huo akiwa na Cruizeiro lakini tukashidwa kutokana na kukosa kibari cha kufanyia kazi England na PSV Eindhoven ikatumia mwanya huo kumnasa."
THOMAS MULLER
"Tulianza kumsikia akiwa na miaka 10 pekee.Tulienda kumtazama lakini kesho yake alisaini kuichezea Bayern Munich"
SERGIO AGUERO
"Wakala wake alitamka bei ambayo hatukuwa tayari kuilipa"
LUKAS MOURA
"Tulitoa £35m lakini Paris Saint-Germain wakamsajili kwa £45m"
MARIO BALOTELLI
"Nilitaka kumsajili mwaka 2010 lakini majibu niliyopata kutoka kwa watu wa karibu yake kuhusu tabia yake yalinifanya niachane na mpango huo kwani ilionekana ni hatari sana kuwa naye kikosini."

0 comments:
Post a Comment