728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 25, 2015

    HII NDIYO TIMU YA EPL AMBAYO PELE ANASEMA ANGEICHEZEA IWAPO UMRI UNGEMRUHUSU

    London,England.


    Mfalme wa soka duniani Pele amesema angetamani kuichezea Arsenal badala ya vilabu vingine vya ligi kuu ya nchini  England.Pele mshindi mara tatu wa kombe la dunia akiwa na Brazil ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na gazeti za The Telegraph la England.

    Pele,74 akijibu swali aliloulizwa kuwa ni klabu gani ya England ambayo angependa kuichezea iwapo angepata nafasi ya kufanya hivyo alijibu Arsenal.
    Arsene Wenger
    Pele ameongeza "Ningechagua Arsenal badala ya Chelsea kwani napenda timu zinazocheza mchezo wa wazi (Open Football).Siku hizi imekuwa ni ngumu kuamua ni klabu ipi inacheza aina hiyo ya soka.
    Lionel Messi celebrates with Neymar after scoring a penalty and Barcelona's third of the game against Levante at the Camp Nou on September 20, 2015
    Mbali ya Arsenal pia Pele ameonyesha kuvutiwa na soka la FC Batcelona na kudai kuwa klabu hiyo ya Hispania inacheza soka linalofanana kwa ukaribu na soka linalochezwa na klabu yake ya zamani ya Santos aliyoichezea miaka ya 1956 na 1974 ama Brazil ya mwaka 1970.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII NDIYO TIMU YA EPL AMBAYO PELE ANASEMA ANGEICHEZEA IWAPO UMRI UNGEMRUHUSU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top